Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemwagiza Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamisi Juma kupitia Tume ya Utumishi wa Mahakama iliyo chini yake kuwachunguza baadhi ya Majaji ambao wamekuwa wakiomba likizo na kusafiri Ulaya kwa zaidi ya siku 28 na familia zao.

 Rais Magufuli ameyasema hayo leo Februari 1, 2018 wakati akihutubia kwenye kilele cha sherehe ya wiki ya sheria nchini iliyofanyika jijini Dar es salaam.

 Amesema kuwa “Kuna baadhi ya watumishi katika sekta ya sheria maadili yao yamepungua, hii ni kweli na ni lazima niseme, wapo wachache.

Ameongeza kwa kusema kuwa  “Katika vibali vya likizo vinavyoombwa na majaji, wapo baadhi yao wanakwenda Ulaya na Afrika Kusini lakini wanaandika watajigharimia wenyewe, lakini wanakaa huko siku 28 au 30 na familia zao wakila kwenye hoteli kubwa kubwa, hizo pesa wanazitoa wapi, nani anawadhamini? Mimi sina majibu, naomba tume yako Jaji Mkuu ichunguze.

Vile vile amesema kuwa “Wapo baadhi watumishi wa mahakama wanaomba rushwa, wanabambikiza kesi wananchi, wanachelewesha kesi, wanaharibu upelelezi, wanachelewesha kuandika kesi na kupendelea. Lakini unaweza kushangaa miongoni mwao walikuwemo mahakimu 26 na walipopelekwa mahakamani wote wakashinda, hakuna hata mmoja aliyepatikana na hatia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *