Mwanamuziki wa Taarab nchini, Isha Mashauzi amewaomba wasanii wote wa kike Tanzania kuachana na mavazi yanayowafanya kubaki utupu na kuwataka wadumishe utamaduni wa kiafrika.
Mashauzi amesema kwamba wasanii wa kitanzania kuvaa mavazi yanayowafanya waonekane utupu kwa madai ya kutafuta soko la kimataifa wanajidanganya kwani kinachoouza siyo video bali ni meseji ya kitu kinachoimbwa.
Isha amedai kwamba video zinasaidia kuwatambulisha wasanii katika jamii ili waweze kufahamiana na mashabiki zao lakini haimaanishi kwamba wavae nguo za uchi katika video zao kwa kuwa hazitoweza kuwasaidia chochote katika maisha yao ya sanaa.
Pia Isha amewasifia wanamuziki wa Taarabu kwa kusema mara nyingi wamekuwa wakiva mavazi ya stara tofauti na wasanii wengine wote na kuwashauri wasanii wengine kutoogopa kuvaa kama wao kwa kuhofia mashabiki au video zao kuacha kuchezwa kwenye Televisheni.