Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mwana FA amesema kuwa katika maisha yake ya kisani hajawahi kuvaa suruali za kubana kama ilivyo kwa wasanii wenzake.
Mwana FA amesema hayo kufuatia kuulizwa kama anapendelea mavazi hayo kama walivya wasanii wenzake.
Mwana FA amesema kuwa tamaduni za Muziki wa Hip Hop ndizo zilizomfanya ashindwe kabisa kuvaa suruali za kubana kwa kuwa kila anapojaribu kuvaa hujikuta anashindwa kupumua.
Amesema kuwa “Unajua nguo zetu sisi watu wa Hip Hop ni ile suruali pana na tisheti kubwa, nimekulia katika mavazi hayo, licha ya kwamba dunia inabadilika lakini mimi nashindwa kabisa kuvaa suruali za kubana kwa kuwa nguo hizo hunifanya nishindwe kuhema,”.
Mwanamuziki huyo huyo kwasasa anatamaba na wimbo unaokwenda kwa jina la ‘Sielewi’ ambao ameuachia hivi karibuni.