Wananchi zaidi ya milioni 25 nchini Tanzania wamedaiwa kuwa hawapati huduma za kimahakama kutokana na upungufu wa majengo ya mahakama na uhaba wa watumishi hususani kwenye mahakama za mwanzo.

Takwimu hiyo imebainika hapo jana  katika uzinduzi wa Mahakama ya Wilaya Bagamoyo wakati Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma alipozindua jengo jipya la kisasa la mahakama ya wilaya mkoani Pwani.

Jaji Mkuu amesema kwamba kukosekana kwa huduma za mahakama karibu ndiyo sababu inayopelekea wananchi kukosa huduma hizo za kisheria, kitendo ambacho kimempelekea kuwataka viongozi wa serikali katika ngazi za mikoa na wilaya kuona mhimili wa huo kama mdau wa serikali katika ustawi wa wananchi kwa kusogeza huduma hizo karibu.

Jaji mkuu amesema maboresho ya mahakama yana lengo la kuongeza idadi ya wananchi watakaopata huduma za mahakama hivyo kujengwa kwa mahakama mpya kutapunguza makali ya uhaba wa mahakama katika maeneo mengi hapa nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Eng. Everest Ndikilo amesema bado kuna changamoto kubwa za katika mahakama za mwanzo na kwani majengo yake hutumika pamoja na taasisi nyingine, jambo linalopelekea kupunguza utulivu katika usikilizaji wa mashauri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *