Muigizaji wa Bongo Movie, Aunty Ezekiel amefunguka kuhusu ishu ya ugomvi wake na mpenzi wake Mose Iyobo.
Aunty Ezekiel na Iyobo wamekuwa kwenye mahusiano sasa kwa muda wa miaka minne name kwa pamoja wamezaa mtoto mmoja anayeitwa Cookie.
Wiki iliyopita Aunty Ezekiel alizua gumzo mtandaoni baada ya kuweka posting yenye utata mtandaoni iliyoashiria kuwa yeye na mpenzi wake Mose Iyobo wapo kwenye migogoro fulani hivi.
Baada ya posti hiyo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii tetesi zilisambaa labda huenda Aunty na Iyobo tayari wameachana kutokana na michepuko.
Aunty alifunguka na kudai kuwa kwenye mahusiano kugombana ni kawaida kwa sababu wote ni binadamu:
Aunty Ezekiel amesisitiza kuwa hapendelei kuanika mambo yake mtandaoni lakini pia hata kwa marafiki kwani hana kawaida ya kuwaambia hata marafiki zake wa karibu mambo yake binafsi.