Msanii wa Bongo Fleva, Rich Mavoko amejikuta anashindwa kujizuia na kuanika penzi lake na msanii mwenzake wa Bongo Fleva Lulu diva.

Rich Mavoko na Lulu Diva wamekataa mara kwa mara habari za wao kuwa na uhusiano wa kimapenzi ingawa habari hizo zimekuwa hazichezi mbali nao kila uchao.

Habari za wawili hawa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi zilianza kusikika tangu mwaka jana ingawa kila mmoja wao amekuwa akikwepa tuhuma hizo na kudai hawana ukaribu wowote bali ni watu walio katika tasnia nyingine.

Lulu Diva
Lulu Diva

Wawili hao walionekana wakiwa wamekaa karibu sana huku mara chache chache walikuwa wakiwekeana mikono kama ishara ya kukumbatiana na kwa wakati huo wakiwa ndani ya maongezi mazito.

Wiki iliyopita habari zilisambaa kuwa Lulu diva kaachwa na sponsor wake anaye muweka mjini kisa ni mahusiano yake na Rich Mavoko lakini kama kawaida yao wawili hao walikataa tetesi hizo na Lulu diva kudai yeye ana mpenzi wake na wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *