Baada ya habari kuenea kuwa mchekeshaji maarufu Bongo, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ kulazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili, muigizaji huyo ameweka wazi ugonjwa unaomsumbua.
Mzee Majuto amesema kuwa alilazwa hospitalini hapo akisumbuliwa na ugonjwa wa tezi dume ambao unamsumbua kwa kipind kirefu.
Mzee Majuto ameanza hatua za awali kuhakikisha kuwa anafanyiwa upasuaji kuondolewa tezi dume linalomsumbua kwa muda mrefu.
Majuto amesema kuwa kutokana na umri wake hashangazwi yeye kupata ugonjwa huo na kudai ni ugonjwa tu kama yalivyo magonjwa mengine hivyo mashabiki wake wasiwe na wasi wasi.
Kwa upande mwingine Mzee Majuto ameshauri watu wengine ambao wana ugonjwa huo wa tezi dume kuhakikisha wanafanyiwa upasuaji mapema kabla ya njia za mkojo kuziba kwani ikifika hatua hiyo watapata shida sana.