Mpenzi wa staa wa muziki nchini Marekani, Nelly aitwae Shantel Jackson amemtetea mpenzi wake huyo baada ya kushtumiwa kumfanyia unyanyasaji wa kingono binti mmoja wakati wa tour yake mwaka jana.

Shantel Jackson ameeleza kuwa mwanadada anayedai kubakwa na rapper huyo sio kweli kwani hata yeye alikuwepo katika eneo la tukio hilo ila alikuwa chumba cha kubadilishia nguo.

Shantel Jackson pia amesema kuwa ni kweli alikuwa amegombana na Nelly lakini hakufanya tendo hilo la ubakaji kwasababu yeye alikuwepo.

Monique Greene  ndiyo  mrembo anayedai kufanyiwa ubakaji na rapper huyo katika gari  la Tamasha maeno ya Washington na sasa wanawake wengine wawili wameibuka na kudai kufanyiwa kitendo kama hicho na msanii huyo.

Nelly anatuhumiwa kwa kumdhalilisha mwanamke huyo kingono wakati wa Tour yake iliyofanyika mwaka jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *