Video queen Bongo ambaye kwasasa amegeukia muziki, Amber Lulu amedai kuwa aliwahi kukataa Tsh. milioni 200 ili apige picha za utupu.

Amber Lulu amedai alikataa kufanya hivyo kwasasa angejidhalilisha kwa jamii kutokana na picha hizo.

Pia amesema kuwa sababu ya iliyofanya kukataa fedha hizo ni kwamba alikuwa ameshaacha kupiga aina hizo ya picha chafu.

Amber Lulu amesema kuwa angechukua hela hizo na kupiga picha hizo ila angeonekana kituko katika jamii na angearibu kazi yake muziki ndiyo mana ameamua kuacha tabia hiyo.

Mwanamuziki huyo alikuwa na sifa ya kupiga picha za utupu na kuweka katika mitandao ya kijamii ila kwasasa ameachana na tabia hiyo baada ya kuingia rasmi kwenye muziki wa Bongo Fleva ambapo anatamba na wimbo wake ‘True Love“.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *