Muigizaji wa Bongo, Wastara Juma amepokea mchango wa kiasi cha milioni 15 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya matibabu ya mguu wake.

Mchango huo umewasilishwa na  Katibu wa Rais, Ngusa Samike nyumbani kwa msanii huyo jijini Dar es Salaam.

Baada ya mchango huo, Wastara amemshukuru Rais Magufuli kwa msaada huo kwa ajili ya matibabu ya mguu wake ambao unamsumbua kila wakati.

Mchango umekuja kufuatia Wastara kuiomba serikali imsaidie kupata matibabu zaidi kwani amedai maumivu makubwa zaidi aliyapata wakati wa kampeni.

Wastara alianza kusumbuliwa na mguu miaka kadhaa iliyopita baada ya kupata ajali ya gari iliyopelekea kukatwa mguu mmoja na hivyo kupelekea ukilema wa mguu mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *