Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu ameingia matatani baada ya kudaiwa kuwafuga wanaume mashoga ndani ya nyumba yake maeneo ya Salasala jijini Dar es Salaam.
Taarifa hizo zinasema kuwa Wema amekuwa akiishi na wanaume hao kwa muda mrefu jambo ambalo limekuwa likiwakera majirani wanaomzunguka na kuwafanya wamshitaki serikali za mitaa.
Muigizaji huyo anadaiwa kuishi na mashoga hao tangu alipokuwa anaishi maeneo ya Ununio jijini hapa hadi kumsababishia matatizo na wakazi wa mtaa huo.
Baadhi ya majirani wa Wema Sepetu wamesema kuwa wanapata wakati mgumu kutokana na mashoga hao kwasasa wana watoto wadogo kwa hiyo wanaweza kuiga tabia za watu hao.
Naye mjumbe wa nyumba kumi katika mtaa wa Salasala, Marko Mbaku amesema taarifa za uwepo wa mashoga amezisikia lakini ameshindwa kupata ushirikiano kutoka kwa muigizaji huyo.