Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesaini mkataba mpya wa miaka miwili na klabu hiyo mpaka 2020.

Mkataba wake wa awali ndani ya klabu hiyo ulitakiwa kumalizika mwakani 2019 lakini ameongeza mpaka 2020.

Baada ya kusaini mkataba huo, Mourinho amesema kuwa anajisikia furaha sana kuendelea kufundisha klabu kubwa kama Manchester United na anashukuru kwa klabu kumuamini aendelee kufundisha timu hiyo.

Kwa upande mwingine Mourinho amemuongelea mchezaji wake mpya Alexis Sanchez ambapo amesema kuwa Sanchez ametoka katika klabu nzuri na kuhamia klabu kubwa ya Manchester United.

Pia amesema kuwa ulikuwa mkataba mzuri kwa kila mmoja na kuthibitisha kuwa Sanchez atajumuishwa katika kikosi cha United cha kombe la FA raundi ya nne dhidi ya Yeovil siku ya Ijumaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *