Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee amefunguka na kusema kuwa alikuwa anakerwa na tabia ya mpenzi wake Jux ya ku-follow wanawake ambao hawaendani nae katika mitandao ya kijamii.
Vanessa ametoa siri hiyo ambayo ilikuwa inamtafuna katika moyo wake kwa kipindi kirefu kwenye mahusiano yake na Jux.
“Wimbo huu ni stori ya ukweli kabisa ambapo mpenzi wangu alikuwa ananikera na tabia ya ku-follow wasichana wengine katika ‘Instagram’ ambao nilikuwa siwataki, siwapendi halafu hatuendani nao. Nikawa namuuliza unawa-follow wa kazi gani ? lakini sikuwa napata majibu sahihi.
Pia Vanessa amedai ameandika wimbo huo kutoka na shida wanazipitia jinsia ya kike (wasichana na wanawake) wanayoipata kwa wapenzi wao pindi wanapotumia mitandao ya kijamii.