Muigizaji wa Bongo Movie, Aunty Ezekiel anasemekana ana matatizoni na mpenzi wake Moses Iyobo ambaye ni mcheza shoo wa Diamond Platnumz.
Aunty Ezekiel na Mose Iyobo wamezaa pamoja mtoto mmoja wa like anayeitwa Cookie, mwanzoni wakati mahusiano yao yanaanza wapo watu wengi sana ambao waliponda kwa kudai kuwa Aunty hana hadhi ya kuwa na mtu kama Iyobo ambaye ni mcheza shoo lakini wenyewe walipendana na walilidhihirisha hilo.
Aunty na Iyobo hawana sana skendo mtandaoni au hawana sana kiki lakini kuna mara chache ambazo Aunty alitumia mitandao ya kijamii kulalama kuhusiana na uhusiano wake na Iyobo.
Miezi michache iliyopita Aunty Ezekiel alitumia ukurasa wake wa Instagram kumlalamikia mwanamke amnaye alikuwa anajigonga kwa Mose Iyobo na alifunguka nakudai kuwa mwanamke huyo alikuwa amedhamiria kumharibia familia yake.
Tangu hapo kumekuwa na tetesi kuwa penzi la Aunty na Iyobo limekuwa likilega lega ingawa hakuna hata mmoj kati yao aliyethibitisha tuhuma hizo.
Jana Aunty aliandika maneno yaliyowapelekea watu wengi kudhani kuwa labda ni kweli penzi lake na baba watoto wake Moses Iyobo liko matatani.