Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mr. Blue amekanusha kuwa na bifu na mwanamuziki mwenzake Diamond Platnumz kama inavyoenezwa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii.
Mr Blue afunguka hayo baada ya kuwepo na taarifa kuwa wawili hao wana bifu ndiyo mana hawajawahi kusapotiana au kuonekana wakiwa pamoja sehemu yoyote.
Kuhusu kufanya kolabo na Diamond, Mr Blue amesema kuwa kolabo na Diamond alishafanya mara mbili ila kama kuna uwezekano wanaweza kufanya tena ila kudhihirisha watu kuwa hawana beef kama inavyokuwa ikienezwa.
Amesema kuwa “Ni mtu nishashirikiana naye sio kitu cha kushangaza labda kusema haiwezekani lakini unajua siku zote mnapokuwa wasanii wakubwa kila mtu anakuwa yupo bize kwa upande wake lakini ikifanyika kolabo ya kati yangu na Diamond ni kitu kizuri kwa sababu tutaonyesha raia hatuna tatizo’.
Blue amesema kuwa hana tatizo na Diamond, ni mdogo wake na anamuheshimu pia anaheshimu hustle zake na amekuwa kama mfano kwa watu, hayo mambo mengine watu wasiyachukulie sana serious,” amesisitiza.
Diamond ameshawahi kumshirikisha Mr. Blue katika ngoma yake inayokwenda kwa jina la kiss to the Lady.