Serikali imeiagiza Klabu ya Simba kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamia suala la uwekezaji kwa Klabu zilizoanzishwa na wanachama ambapo inawataka kuchukua 51% na mwekezaji  49%.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe alipokutana na uongozi wa Klabu ya Simba na kuzungumza nao kufuatia kutoa asilimia 50% kwa mwekezaji wa klabu hiyo Bw. Mohamed Dewji waliyemtanganza hivi karibuni ambapo ni kinyume na sheria.

Amesema kuwa “Kanuni zinazosimamia masuala ya udhamini kwa vilabu zilifanyiwa marekebisho Novemba  2017 ambapo ilioneka ni vyema klabu za michezo zilizoanzishwa na wanachama wanapopata mwekezaji basi achukue 49% na wanachama wapewe 51% lengo ikiwa ni mwanachama aweze kunufaika vizuri,”.

Kwa Upande wa Kaimu Rais wa Klabu ya Simba Bw. Salim Abdallah ameishukuru serikali kwa kuwafungulia milango pale watakapo kuwa na tatizo au watakapo hitaji ushauri na kuahidi kuzingatia maagizo ya Waziri pamoja na matakwa ya sheria hiyo ya uwekezaji kwa vilabu.

Disemba 3, 2017 klabu ya Simba kupitia mkutano wake mkuu uliofanyika jijini Dar es salaam ilimtangaza Mfanyabiashara Mohamed Dewji kama mshindi wa zabuni ya kuwekeza ndani ya klabu hiyo kwa dau la shilingi bilioni 20.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *