Mwanamuziki wa dansi nchini, Papii Kocha amefunguka na kudai maisha ya uraiani ni sawa na dunia nyingine kwani mtu akiwa anatumikia adhabu ya kifungo gerezani huwa vitu vingi vizuri anashindwa kufanya.
Papii ameeleza hayo pindi alipokuwa kwenye matayarisho ya ujio wake mpya katika muziki akiwa pamoja na Baba yake Nguza Viking maarufu kama Babu Seya ambapo wawili hao walitoka jela kwa msamaha wa Rais Magufuli.
Papii amesema kuwa “Miaka 14 siyo mchezo, mambo kama haya si unayaona mwenyewe, niliya-miss, nime-miss vitu vingi, picha za ukweli, mambo haya kule tulipotoka hamna. Lazima uelewe hii ni dunia nyingine”.
Pamoja na hayo, Papii ametoa ahadi kwa mashabiki na wapenzi wa ‘dance’ kwa kuwapa kitu kilichokuwa bora zaidi tofauti na zile walizokuwa wamezifanya kipindi cha awali.
Papii Kocha na baba yake, Nguza Viking maarufu kama babu Seya kwasasa wapo huru baada ya kutoka jela kwa msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.