Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Sam wa Ukweli amefunguka sababu iliyosababisha kukaa kimya kwenye game la muziki wa Bongo Fleva.
Sam wa Ukweli amesema kuwa ukata ulioivamia kampuni iliyokuwa inasimamia kazi zake za muziki ulisababisha akwame kuendelea na sanaa kwa muda.
Mwanuziki huyo amesema baada ya kuona wasimamizi wake wamekumbwa na ukata huku akiwa amefungwa pingu ya mkataba wa miaka mitatu, aliona asiingie kwenye mgogoro wa kimkataba kama ilivyokuwa kwa Diamond Platinumz.
Baada ya kuona muziki unaenda kombo kwa upande wake akaamua kujikiti kwenye kilimo cha mananasi nyumbani kwao Kiwanga Bagamoyo mkoani Pwani.
Sam wa Ukweli alitamba na nyimbo kama vile ‘Sina Raha’ pamoja na ‘Hata Kwetu Wapo’ ila kwasasa ameachia ngoma mya inakwenda kwa jina la ‘Milele’.