Rais mteule wa Liberia, George Opong Weah leo anatarajia kuapishwa kuwa rais wa nchi hiyo kwenye sherehe zitakazofanyika nchini humo.
Weah anaapishwa leo baada ya kumshinda aliyekuwa makamu wa rais wa nchi hiyo kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana.
Weah aliingia katika siasa baada ya kustaafu soka mwaka 2002 na akawa miongoni mwa maseneter katika bunge la Liberia.
Aligombea urais mwaka 2005 na Alimshinda na Bi Johnson Sirleaf wakati wa duru ya kwanza katika uchaguzi huo lakini kashindwa katika duru ya pili ambapo kambi yake ilisusia kushiriki katika duru ya pili.
Aliyewahi kuwa meneja wa George Weah katika klabu ya Monaco inayocheza ligi kuu ya Ufaransa Arsernal Wenga amealikwa na atakuwepo katika uapisho huo.
Meneja huyo wa Arsenal alikuwa meneja wa Weah katika klabu ya Monaco inayocheza Ligi Kuu ya Ufaransa miaka ya 1990 na amesema hakuwahi kufikiria kwamba wakati mmoja mchezaji huyo angekuwa rais.