Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimebadili msimamo wake wa kususia uchaguzi mdogo na kuamua kuwatangaza wagombea katika majimbo ya Kinondoni na Siha.

Awali, Chadema na vyama vinavyounda Ukawa vilisusia uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo ya Longido, Songea Mjini na Singida Kaskazini kwa madai kuwa hawakuridhishwa na mazingira ya uchaguzi wa Udiwani katika Kata 43 uliofanyika Novemba 26 mwaka jana.

Aidha, vyama hivyo vilitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kusitisha uchaguzi huo ili kutoa fursa ya kukutana na kutoa tathmini ya mazingira ya uchaguzi jambo ambalo tume ililipinga kwa kusema kuwa inasimamia sheria.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa Chama hicho hakikusema kuwa hakitashiriki bali walitoa sababu kwamba hawakuridhishwa na uchaguzi mdogo wa kata 43.

Mbowe amesema kuwa “Kilio chetu kimesikika ndani na nje ya nchi, kimesikika kwa wananchi, kwa hatua hiyo hiyo tumeona hatutawatendea haki wananchi wa Kinondoni na Siha ambao wamewekewa wagombea ambao hawawataki na hilo kila mtu analijua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *