Muigizaji nyota wa Hollywood, Lupita Nyong’o anatarajia kuchapisha kitabu chake cha kwanza kuhusu watoto kiitwacho ”Sulwe” hivi karibuni.
Sulwe ikimaanisha ‘nyota’ kwa lugha ya Kijaluo ni hadithi ya mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitano ambaye amelelewa nchini kenya.
Katika kitabu hicho , Sulwe ni msichana mweusi katika familia yake, swala linalomfanya kuwa na wasiwasi na sasa ameamua kutafuta njia ya kung’arisha ngozi yake na kuwa mweupe.
Huku habari hiyo ikiendelea, Sulwe anaanza safari ambayo kupitia ushauri wa mamake inamsaidia kuelewa urembo kwa njia tofauti.
Kwa Bi Nyongo, uamuzi wa kugusa ama kuzungumzia kuhusu mada hii nzito katika kitabu cha watoto ulikuwa wazi.
Hadithi hiyo inapanda mbegu katika akili ya wototo , hatua inayoruhusu watoto kupata mafunzo ambayo hawayatambui wakati wanaposoma vitabu, alisema bi Nyongo katika mahojiano.
Wakati anapofikiria kuhusu safari yake ya kuikubali nafsi yake na kujipenda, bi Nyong’o anasema kuwa hatua yake ya kusoma na mamake ilimsaidia sana katika ukuwaji wake.
Baadaye alitumia tamko lake kuwasilisha ujumbe mkali kuhusu umuhimu wa rangi na uwakilishaji katika Hollywood na kwengineko.