Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nikki wa Pili amelitaka Baraza la Sanaa nchini kuzingatia suala la maadili kwa pande zote na siyo mavazi pekee.
Kauli hiyo ya Nikki wa Pili imekuja kufuatia Baraza la Sanaa (BASATA) kufungia baadhi ya wasanii wa kike kutoka na kuvaa mavazi yasiyokuwa ya maadili kwa jamii.
Nikki wa Pili ambaye ni memba wa kundi la Weusi amesema kuwa baraza linatakiwa kuangalia swala la maadili kwa upana sana na sio katika mavazi tu kwa sababu hata kwa upande mwingine ukiangalia utakuta kuwa hata wao kama baraza wanakuwa hawatimizi majukumu yao wa wasanii.
Nikki amesema kuwa Baraza wanakosea wanapokuwa wanawafungia wasanii tena hasa wa kike kwa sabau ya maadili ili hali wanapaswa kuangalia vitu vigni kabla ya kutoa uamuzi huo.
Wasanii hao wamefungiwa baada ya kuweka video na picha chafu katika mitandao ya kijamii na kutoa ahadi kuwa yeyeto atakae toa wimbo usiokuwa na maadili ya kitanzania basi wimbo huo na kazi zake zitafungiwa.
Wasanii waliofungiwa hivi karibuni kutokana na utovu wa nidhamu katika kazi za muziki ni pamoja na Gigy money na Pretty kindy huku wengine wakiambiwa kuripoti katika ofisi za baraza lakini pia wimbo wa Rostam wa Kibaa100 pia umefungiwa mpaka utakapofanyiwa marekebisho katika baadhi ya vipengele.