Mwanamitindo wa kimataifa nchini Marekani, Amber Rose anatarajia kufanya upasuaji wa matiti yake ili kuyapunguza.
Amber Rose amesema kuwa amechoshwa na ukubwa wa matiti yake na ameamua kutilia mkazo suala lake la kuyapunguza ili yaweze kuendana na mwili wake kama yeye mwenyewe alivyodai.
Kwa mujibu wa mtandao wa Page Six imeelezwa kuwa baby mama huyo wa Wiz Khalifa na girlfriend wa rapper 21 Savage, atafanyiwa upasuaji wa kifua chake na Dr. Garth Fisher mapema leo.
Dkt. Fisher ameeleza kuwa Amber anahitaji kupunguza matiti hayo ili aweze kuwa huru katika kazi zake.