Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Recho amekanusha taarifa kuwa mwanamuziki mwenzake T.I.D ndiyo aliyemfundisha kutumia dawa za kulevya.
Recho amesema kuwa watu wamekwa wakisema maneno mengi kuhusu yeye kujiingiza kwenye masuala ya madawa ya kulevya wakati hawajui ukweli wowote.
Kuhusu kupotelewa sDubai, Recho amesema kuwa sio kweli na kwamba alipokuwa anaenda Dubai alikuwa ameenda katika shughulli zake za kikazi na alikuwa ana uwezo wa kujimudu na hata huyo mwanaume alimpata alipokuwa huko na walikuwa wakiishi vizuri bila matatizo yoyoyte tofauti na watu wanavyosema kuwa alikuwa akiishi maisha ya shida.
Recho amesema kuwa alikuwa na passport yake na wala haikuwa imeisha muda, lakini pia hakwenda Dubai na mwanaume na wala hakuwa anamtegemea mwanaume yoyote, lakini pia mwanaume aliyekutana nae Dubai hakuwahi kumtesa wala kumtelekeza.
Recho amesema kuwa mara nyingi alikuwa akikaa kimya na hakutaka kuposti kitu chochote katika mitandao kwa sababu watu wengi walikuwa wakimuuliza kwanini yupo kimya na alikwa akishindwa kuelezea sababu ya kukaa kimya kwa sababu hata yeye alikuwa anaumia sana anapokumbuka kuwa kilichomfanya mpaka kukaa kimya kwenye muziki kilikuwa kikimuumiza.
Recho anasema kuwa amekuwa akikaa ndani muda mrefu kwa sababu alikuwa akikaa ndani kwa muda mrefu kwa sababu watu walikuwa wakimtenga na alikuwa akijifungia ndani muda mrefu kwa sababu hata sehemu ya kuomba ela haikuwepo watu wanakupa ahadi lakini hawakupi ela.