Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego amelaani kitendo cha watu wasiofahamika kudukua acount zake za instagram na Youtube, na kufuta vitu vyake vyote.
Nay amesema watu hao walianza na acount yake ya instagram na kisha kuingia Youtube, na kufuta kazi zake zote alizofanya tangu anaanza muziki.
Nay amesema kuwa “Yaani wamehack acount yangu ya instagram, ilikuwa na followers zaidi ya milioni moja, usiku wakaingia kwenye YouTube wakafuta kazi zangu zote, yani mtu anafuta vitu bila huruma, sijui kwa nini tunachukiana hivi, wasanii wenyewe tupo wachache lakini tunachukiana hivi”.
Kufuatia tukio hilo Nay wa Mitego amesema tayari amezungumza na mtaalamu wa masuala ya mtandano Mx Carter, ili kumrudishia acount zake.
Nay wa Mitego si wa kwanza kulalamikia suala hilo la udukuaji akaunti za mitandaoni ya kijamii, hivi karibuni Baraka The Prince pia alilalamika kufanyiwa mchezo mchafu kwenye akaunti yake ya Youtube.