Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amemaliza mgogoro wa ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara ambao umedumu kwa miaka mitatu.

Waziri Mkuu ametoa uamuzi huo Januari jaan wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime pamoja na Halmashauri ya Mji wa Tarime.

Amesema amesitisha mpango huo wa ujenzi wa makao makuu ya halmashauri hiyo kwa kuwa imepangwa kujenga katika eneo ambalo lipo mbali na wananchi.

Pia, Majaliwa amesema Serikali haiwezi kuruhusu ujenzi huo ufanyike katika eneo ambalo ni mbali ya makazi ya wananchi kwa kuwa watashindwa kufuata huduma.

Aidha, amesema Serikali itapeleka wataalamu watakaofanya uchunguzi na bainisha eneo sahihi la kujenga Halmashauri hiyo kwa kutumia ramani.

Waziri Muu pia amewataka watumishi wa umma kutotamani fedha za maendeleo zinazotolewa na Serikali ajili ya miradi ya maendeleo.

Amesisitiza kwamba wasipokuwa makini na fedha hizo zitasababisha wachukuliwe hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuondolewa kazini. ”Je mpo tayari kuchukuliwa hatua.?

Amesema Serikali inapeleka fedha kwenye halmashauri kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maendeleo ya wananchi na si kuwanufaisha watu binafsi.

Pia amewataka watumishi kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wawe wabunifu na wajue halmashauri zao zinahitaji nini ili kuweza kusonga mbele kimaendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *