Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amepiga marufuku aina yoyote ya michango katika shule za Serikali za msingi na Sekondari.
Marufuku hiyo ya Rais Magufuli imekuja kufuatia baadhi ya shule za msingi na Sekondari kuchangisha wanafunzi michango wawapo shuleni.
Rais Magufuli pia amewaagiza Mawaziri Suleiman Jafo na Joyce Ndalichako kusimamia suala hilo kikamilifu zaidi.
Rais Magufuli amepiga marufuku hiyo hiyo leo alipokutana na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani S. Jafo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce L. Ndalichako Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Magufuli amewataka mawaziri hao kwenda kusimamia jambo hilo na kuhakikisha hakuna michango yoyote wanafunzi au wazazi wanachangishwa kwenye shule za msingi na sekondari.