Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa amefungukiwa mechi tatu na kulipa faini ya Tsh. 500,000 kutokana na kosa la kumpiga mchezaji wa Tanzania Prisons kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kamati ya nidhamu iliyokutana jana Jumapili, Januari 14, 2018 imepitia kesi ya mshambuliaji huyo iliyowasilishwa na Bodi ya Ligi.

Chirwa alishtakiwa kwa kosa la kumpiga mchezaji wa Tanzania Prisons kwenye mchezo huo uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1. Chirwa ambaye alifika kusikiliza kesi hiyo akiwa na mwakilishi wake alikiri kutenda kosa hilo.

Kamati baada ya kumsikiliza Chirwa na kupitia Video za mchezo huo pamoja na taarifa ya kamishna  na Muamuzi imetoa adhabu kwa mchezaji huyo kupitia Kanuni za Ligi Kuu kanuni ya 37 (7b) na kanuni za nidhamu za TFF kifungu cha 48(1d) na 48(2).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotelewa na TFF, adhabu hiyo imetolewa baada Chirwa kukiri kufanya kosa hilo la kumpiga mchezaji wa Tanzania Prisons.

Michezo mitatu ambayo Chirwa ataikosi ni dhidi ya Mwadui, Njombe Mji na Majimaji mechi zote zitafanyaika kwenye uwanja w Uhuru.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *