Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Pinki amefunguka na kukiri kumlazimisha msanii mwenzake Chemical watengeneze kiki kwa ajili ya wimbo wao mpya.
Wasanii hao wawili walishika headlines kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuingia kwenye bifu siku chache zilizopita na kuanza kurushiana maneno mtandaoni.
Pinki amethibitisha kuwa haikuwa rahisi kumshawishi Chemical kukamilisha misheni hiyo ambayo yeye amedai kuwa wazo la kiki ni lilitolewa na uongozi wake ambao ulishauri lakini amekiri kiki imesaidia kupush wimbo huo aliomshirikisha Chemical.
Pia Pink amesema kuwa hii idea ilitoka kwa management yake na kusema kweli haikuwa rahisi kumshawishi Chemical kwasababu yeye siyo mtu wa kiki.
Lakini na Chemical amefunguka na kudai kile alichofanya silo kitu ambacho amekizoea bali ilikuwa ni mara ya kwanza yeye kufanya hivyo na pia amedai badala ta kumtukana mashabiki wake wa ukweli walimfata inbox na kumhoji kulikoni yeye na kujibizana na watu mjtandaoni.