Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amekanusha tetesi za kutoka kimapenzi na mwanamuziki mwenye asili ya Congo, Mohombi.
Wema amesema kuwa habari hizo si za kweli tena ila watu wameamua kumzushia pasipo kujua ukweli juu ya issu hiyo.
Mohombi alikuwepo nchini Tanzania katika uzinduzi wa album ya msanii wa Vannesa Mdee ambapo kuna baadhi ya nyimbo wameimba wote.
Hata hivyo katika watu waliopata kuwa karibu na msanii Mohombi na kupiga nae picha ni Wema Sepetu ambapo baada ya picha hizo kuonekana katika mitandao ya kijaimi ilianza kusambaa kuwa msanii huyo ametoka kimapenzi na Wema Sepetu.
Pia Wema amesema kuwa kitendo cha kupiga picha na Mohombi ni kawaida kwa sababu ni shemeji yake na ana uhusiano na mtu wake wa karibu na ipo siku akiamua atamueka wazi mtu huyo.
Wema amekuwa ni moja ya mastaa wa kike wachache ambao wanakumbwa sana na tuhuma za kujiingiza katika mapenzi na wasanii wengi wakubwa na kutokudumu nao katika mahusiano.