Naibu Waziri wa Ofisi ya makamo wa Rais anayeshughulikia muungano na mazingira, Luhaga Mpina ametoa wito kwa taasisi za muungano zinazofanya tafiti za kisayansi kufanya tafiti hizo kuwa za tija kwa serikali na Umma.
Naibu waziri huyo aliyasema hayo alipotembelea taasisi ya muungano ya sayansi ya bahari ya chuo kikuu cha Dar es Salaam iliyopo katika mji wa Magharibu B visiwani Zanzibar iliyopo chini ya wizara ya Elimu, Sayansi na teknolojia.
Mpina alishauri tafiti za taasisi hiyo ziwe zenye malengo za kusaidia watanzania waishio ukanda wa pwani ili kuwawezesha kuinua uchumi wao na kuongeza pato la taifa.
Vile vile naibu waziri huyo ameongeza kwa kusema kwamba anategemea tafiti zainazofanywa na taasisi hiyo zitoe mwongozo kwa serikali kwa maana ambayo nchi inavyoweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Taasisi hiyo imekuwa ikitoa nafasi kwa wanafunzi wageni kutoka nchi mbalimbali duniani kuja na kufanya tafiti juu ya viumbe hai waishio baharini aina ya dolphin ili kuweza kufahamu mazingira na tabia za ndani za viumbe hao na kubadilishana uwezo wa kuongeza kipato kwa taasisi hiyo kupita malipo ya mafunzo hayo.