Rais wa Marekani amewashutumu wahamiaji wanaoingia nchini humo kwa kuwatusi katika afisi yake ndani ya Ikulu ya Whitehouse.
Rais Trump aliwaambia wabunge siku ya Alhamisi kulingana na gazeti la The Washington Post.
Ikulu ya Whitehouse haikukana tamko hilo ambalo lilithibitishwa na vyombo vyengine vya habari.
Kama mataifa mengine ambayo yana wahamiaji wanaofaa kuwa nchini humo, rais Trump anapigania suluhu ya kudumu inazofanya taifa hilo kuwa thabiti kwa kuwakaribisha wale ambao wana mchango katika jamii ,hukuza uchumi wetu na kuingiliana na raia wa taifa letu.
Kamwe hatakubali mkakati wa muda mfupi ulio hafifu na hatari ambao unahatarisha maisha ya raia wa Marekani, mbali na kutowaruhusu wahamiaji wanaotaka maisha mazuri Marekani ijapokuwa kupitia njia halali.
Matamshi hayo ya rais Trump yanajiri huku wabunge kutika vyama vyote wakimtembelea kupendekeza mpango wa wahamaiji usiopendelea upande wowote.
Seneta wa Democrat Richard Durbin alikuwa akizungumza kuhusu vibali vya muda wa kuishi vinavyotolewa kwa raia wanaotoka katika mataifa yaliokumbwa na majanga, vita ama milipuko ya magonjwa, vilisema vyombi vya habari.
Kulingana gazeti la Washington Post , bwana Trump aliwaambia wabunge kwamba Marekani badala yake inachukua wahamiaji kutoka Norway, ambayo waziri wake mkuu alimtembelea rais Trump siku ya Jumatano.
Seneta Lindsey Graham, ambaye ni mwanachama wa chama cha Republian kutoka Carolina Kusini pia alikuwa katika mkutano huo lakini hakuweza kuzungumzia kuhusu matusi hayo yaliotolewa na rais Trum.