Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage amedai kuwa kama klabu hiyo haijatatua matatizo yake uenda wakakosa ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu.

Rage ameyasema hayo baada ya klabu hiyo kuondolewa kwenye Kombe la Mapinduzi huku pia ikiwa imeshaondolewa kwenye Kombe la FA.

Rage amesema licha ya Simba kuwa vinara wa ligi kwa sasa, lakini kama viongozi, wachezaji na benchi la ufundi hawatakuwa na umoja, timu itavurugana zaidi na kushindwa kufikia malengo.

Amesema kuwa “Ukiangalia Simba ya msimu huu naona kama imerudia makosa ya Yanga waliyowahi kuyafanya huko nyuma, wamesajili wachezaji wengi bila ya kuangalia uhitaji wa timu zaidi ya kuangalia majina tu. Hili ni tatizo.

Pia amesema kuwa “Tatizo lingine ninaloliona ndani ya Simba mpaka kusababisha kufanya kwao vibaya ni kutokuwa na umoja baina ya wachezaji, benchi la ufundi na viongozi, wanatakiwa kukaa chini na kumaliza tofauti zao haraka kabla hatari zaidi haijatokea. Kugombana kumepitwa na wakati.

Ameongeza kwa kusema kuwa “Haiwezekani leo hii eti wachezaji wanafanyiwa mabadiliko halafu wanaondoka kwenye benchi, huu ni utovu wa nidhamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *