Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa itakuwa furaha kutetea wadhfa wake wa urais dhidi ya aliyekuwa nyota wa kipindi cha mazungumzo nchini Marekani Oprah Winfrey.

Trump ametoa kauli hiyo wakati akiwajibu maripota wakati wa mkutano kujadili mabadiliko ya sheria za uhamiaji na maseneta wa Marekani.

Mwanawe wa kike Ivanka Trump alijiunga na raia wengine wa taifa hilo kusifu hotuba ya Oprah wakati wa tuyo za Golden Globe.

Mwandani wa Winfrey amesema muigizaji huyo ‘havutiwi’ na uwezekano wa kutangaza kuwania urais 2020.

Hotuba yake kuhusu umuhimu wa kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia ilivutia pongezi kutoka kila eneo la Marekani.

Trump alisema wakati wa mkutano wake siku ya Jumanne kwamba kampeni dhidi ya bi Winfrey itakuwa ya kufurahisha sana.

Alikuwa na Trump na familia yake. Nampenda sana Oprah lakini sidhani kwamba atawania urais.Nilimjua sana.

Miongo miwili iliopita katika CNN, bwana Trump alisema kwamba iwapo atawania urais basi atamchagua bi Winfrey kuwa mgombea mwenza .”Oprah.

Mwaka 2015 – wiki moja kabla ya kutangaza kuwa atawania urais-bwana Trump alisema kuwa angependelea kumchagua bi Oprah kuwa makamu wake wa urais.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *