Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Hussein Jumbe amesema kuwa alikutana na Rayvanny kwa ajili ya mazungumzo kabla ya Rayvanny kurudia wimbo wake wa Siri.

Hussein Jumbe amesema kuwa katika kurudia wimbo huo, Rayvanny na uongozi wake walimwita na kuongea nae vizuri na kumlipa kiasi cha pesa kizuri ambacho ameridhika nacho na kumruhusu kufanya wimbo huo kwa amani kabisa.

Pia  mwanamuziki huyo aliyewahi kutamba na bendi za Sikinde na Msondo Ngoma amesema kuwa amefurahi kuona Rayvanny ameutendea haki wimbo huo.

Ameongeza kwa kusema kuwa sababu kubwa ya kukubali Rayvanny kufanya wimbo huo ni kwa sababu anajua kuwa kundi la Wasafi na wasanii wake wanafanya kazi nzuri.

Vile vile ametoa shukrani zake za dhati kwa lebo ya wasafi na kusema kuwa anaona fahari kuona wamemkumbuka na kuukumbuka wimbo wake kwa sababu watu wengi wamekuwa wakiupa kisogo wimbo huo.

Wimbo wa Jumbe ‘Mapenzi ya Siri’ ulitoka mwaka 2001 na hata wimbo wa Rayvanny alishauri uitwe mapenzi ya siri lakini wakaona bora wauite siri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *