Hakimu mmoja nchini Brazil ameruhusu maandamano ya amani ya kisiasa wakati wa michezo ya olimpiki inayoendelea mjini Rio, Brazil.
Maamuzi hayo yamekuja baada ya waandamanaji hao kufukuzwa katika viwanja mbalimbali vya olimpiki kwa kubeba mabango ya kumkosoa Rais wa mpito, Michael Temer.
Hakimu huyo amesema kuwaondoa waandamanaji hao ni ukiukwaji wa uhuru wa kujieleza kwa hiyo sheria inasema ruksa kwa wanamandaji kuandamana kwa amani.
Amepokea maombi ya kuruhusu maandamano hayo kutoka kwa chombo cha serikali cha kutetea maslahi ya umma, hata hivyo waandaji wa michezo ya Olimpiki wanatarajia kupinga uamuzi huo.