Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu leo asubuhi ameondoka kutoka katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya na kwenda nchini Ubelgiji kwa matibabu zaidi.

Lissu amepelekwa na Ndege ya Shirika la Kenya akiambatana na mke wake, Alicia ambapo amesindikizwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta na watoto wake pacha, Augustino na Edward, ndugu zake, viongozi na wanachama wa Chadema.

Kuhusu gharama, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji amesema gharama za safari na matibabu zimegharamikiwa na Chadema pamoja na TLS. Miongoni mwa waliokuwapo hospitalini kumsindikiza Lissu uwanjani hapo kaka yake Alute Mghwai, mdogo wake, Vincent Mghwai, Dk Mashinji, John Mnyika (Bara), Salum Mwalimu, Susan Kiwanga (Mlimba), Godbless Lema (Arusha Mjini), John Heche (Tarime Vijijini), Rose Kamili (Viti Maalum), Anna Gideria (Viti Maalum) na ndugu wengine.

Lissu ametoka hospitalini hapo ikiwa baada ya matibabu aliyoyapata tangu Septemba 7 mwaka jana baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana kwenye makazi yake Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *