Baba mzazi wa msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Mzee Abdul Juma amemjia juu mzazi mwenzake mama Diamond ‘Bi.Sanura’ kuacha vijembe vyake mara moja anavyompiga Hamisa Mobetto.

Tangu Diamond azae na Hamisa na aweke wazi kabisa kuwa hawezi kumuacha mzazi mwenzake Zari kumekuwa na bifu kali ambalo limekuwepo kati ya Hamisa na Zari kwa muda mrefu sasa lakini wiki iliyopita walimalizia hasira zao mtandaoni kwani kila mmoja alimrushia mwenzake maneno mazito mtandaoni.

Katika kipindi chote hiki Mama Diamond amekuwa akionyesha waziwazi kuwa yupo upande wa Zari na huwa mara kwa mara hupendelea kumpiga vijembe Hamisa wazi wazi.

Baba Diamond amemchana Mama Diamond na kumtaka kuwa na busara na aache kuchagua upande mmoja ambao anaunga mkono.

Lakini pia Baba Diamond amewatolea povu Zari na Hamisa kwa kitendo chao cha kurushiana maneno ya kejeli mtandaoni na kudai wanaibisha wao kama wazazi badala yake amewataka Zari na Hamisa wakae kimya na kila mmoja afanye mambo yake na yeyote atakayeanza kunyamaza huyo ndio atakuwa mke wa kuoa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *