Mwanamuziki nyota wa dansi nchini, Christian Bella amekanusha vikali taarifa iliyomkumba ya utumiaji wa dawa za kulevya.

Bella amekanusha taarifa hizo baada ya kuzambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba msanii huyo anatumia madawa ya kulevya.

Taarifa hizo zilsema kwamba kuwa wana taarifa za kumshuhudia msanii huyo anatumia unga/ madawa ya kulevya.

Bella amesema kuwa tuhuma hizo hazina mashiko yoyote kwa habari hizo zinasambazwa na watu wasiomtakia mema.

Pia Bella amesena hawezi kujiingiza kwenye anasa ya kutumia madawa ya kulevya kwani anajua mwisho wake na yeye anajielewa majukumu yake.

Bella amewahakikishia mashabiki zake kuwa kamwe hawezi kujiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya na sababu alikosa kufanya show mbili ni alikuwa anaumwa na walasio uteja kama ilivyozushwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *