Kiungo wa timu ya Liverpool ambaye ni raia wa Misri, Mohamed Salah ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika wa mwaka 2017.
Salah alikuwa akishindana na Pierre-Emerick Aubameyang, na Sadio Mane na akaibuka mshindi bora zaidi kwa wingi wa kura na ubora awapo kiwanjani.
Mane na Salah walihudhuria sherehe za kutangazwa kwa washindi mjini Accra, Ghana saa 24 kabla ya mechi ya Kombe la FA Ijumaa ambapo klabu yao ya Liverpool itacheza dhidi ya Everton.
Salah alionekana kuitetea vyema timu yake ya Liverpool mwaka 2017 baada ya kujipatia goli 23 katika mechi 29 baada ya kujiunga katika ligi kuu ya England akitokea timu ya AS Roma.
Wapinzani wake nao si haba kwani Pierre-Emerick Aubameyang, wakati huo huo, alifunga mabao 31 ya kipekee kati ya michezo 32 katika mashindano yote ya mwisho.
Tuzo hiyo ya shirikisho la soka barani Afrika ilikuwa na orodha ya wachezaji wapatao 24, lakini mwezi Desemba Salah, Aubameyang na Mane walitangazwa kuingia katika hatua ya mwisho ya tatu bora .
Mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka uliopita alichaguliwa na makocha kwa kushirikiana na manahodha wa timu katika kila timu ya wanaume ya taifa barani Afrika.
Mwenzake Sadio Mane kutoka katika timu ya Liverpool Sane alikuwa mshindi wa pili kwa wingi wa kura, naye nyota mchezaji wa timu ya Dortmund, Aubameyang akaushika nafasi ya tatu kwa wingi wa kura.
Wengine waliopata tuzo hiyo ni Mwanasoka bora wa kike wa Afrika Asisat Oshoala (kutoka Nigeria)
Aidha tuzo nyingine inayoitwa Platinum Award ilikwenda kwa marais wawili barani Afrika ambao Nana Akufo-Addo Rais wa Ghana na George Weah Rais Mteule wa Liberia na mwanasoka bora ya Afrika bara la ulaya.