Baba mzazi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Mzee Abdul amewataka Zari na Hamisa Mobeto waache kurushiana vijembe kwani hakuna mke halali wa mtoto wake.
Kauli ya baba mzazi wa Diamond inakuja kufuatia wanawake hao kulumbana na kutupiana maneno ya kejeli katika mitandao ya kijamii kila mmoja akijiona zaidi ya mwenzake.
Mzee Abdul ameingilia kati malumbano kati ya wawili ambao wote wamezaa na mwanae Diamond Platinumz.
Mzee huyo amesema kuwa maneno wanayotoleana mitandaoni ni mabaya na yanamchukiza mno kwasababu kila mmoja hakuna mwenye ndoa na mtoto wake.
Pia amesema kuwa anawasihi wanawake hao waache malumbano katika mitandao ya kijamii, kwa sababu kila mmoja amezaa hivyo wote wana nafasi na haki sawa kwa vile hakuna aliyeolewa hadi sasa.
Ameongeza kwa kusema kuwa mwanaye bado hajaoa na huenda mmoja wao akaolewa lakini mwingine akapewa heshima yake kama mzazi.
Amesisitiza kuwa kua uwezekano mkubwa kwa wote wawili kuolewa kwani dini ya mwanae inamruhusu.