Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amefunguliwa amshtaka na Chama cha Soka England (FA) kutokana na tamko lake kuhusu waamuzi baada ya mechi yao ugenini Jumapili kumalizika 1-1 ugenini dhidi ya West Brom.
Wenger alikasirika baada ya mwamuzi Mike Dean kuwapa West Brom mkwaju wa penalti, ambapo walifunga na kusawazisha.
Inadaiwa kwamba aliyoyatenda Wenger, 68, katika chumba cha kubadilishia mavazi cha waamuzi baada ya mechi yalikuwa matusi na ya kukera na kwamba alitilia shaka maadili na uwezo wa mwamuzi.
Huku mechi ikiwa imesalia dakika moja kumalizika The Hawthorns, Arsenal wakiongoza 1-0, Calum Chambers aliadhibiwa baada ya Kieran Gibbs kuusukuma mpira na ukagusa mkono wake.
Sheria za soka zinasema adhabu inafaa kutolewa tu iwapo mchezaji alinawa mpira makusudi na kwamba umbali kati ya mchezaji mpinzani na mpira unafaa kuzingatiwa.
Chambers alikuwa amesimama mita mbili hivi kutoka kwa Gibbs.
Akizungumza Jumanne kabla yake kushtakiwa, Wenger alisema: “Inasikitisha sana.
“Linalosikitisha zaidi kwangu ni kwamba hilo limefanyika mara nyingi msimu huu – Stoke, Watford, Man City, na sasa West Brom.
Januari, alipigwa marufuku kutokuwa uwanjani mechi nne baada ya kupatikana na hatia kumhusu mwamuzi Anthony Taylor mechi ya ligi dhidi ya Burnley.
Arsenal, walio nafasi ya tano Ligi ya Premia kwa sasa, watakutana na Chelsea walio nafasi ya tatu Jumatano.