Mwanamuziki mkongwe wa hip hop nchini, Jay Moe amefunguka sababu ya muziki huo kushindwa kufanya vizuri zaidi kimataifa.

Jay Mo amesema kuwa sababu ya wasanii wengi wa hip hop kushindwa kufanya vizuri kimataifa ni kutokana na kufanya kazi nje ya lebo.

“Wengi wanafanya muziki wao nje ya label, kwa hiyo leo ukitaka kumfananisha Fid Q ambaye hayupo kwenye label yoyote zaidi ya Cheusi Dawa ambayo anaimiliki mwenyewe leo tukamfananishe na Mr. Incredible ambaye yupo chini ya Chocolate City au Fino, Cassper Nyovest  hao wameshajitangaza,”.

Jay ameongeza kuwa kuna nchi nyingine hakuna utaratibu wa label lakini kuna kampuni kubwa ambazo zinawekeza katika muziki huo kitu kinachofanya kuendelea kukua.

Pia ameongeza wasanii hip hop wenyewe wameshindwa kutengeneza maudhui ya kibishara ambayo yanaendana na soko la sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *