Umoja wa Mataifa umemwambia Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila kutimiza ahadi aliyoiweka ya kuachia madaraka na kupisha uongozi mwingine.
Rais Kabila mwenye miaka 46, ameiongoza DRC kwa miaka 17 na msimu wake wa mwisho wa uongozi uliisha tangu December 31, 2016 na akatakiwa aachie ngazi lakini uchaguzi wa kupata Rais na viongoi wapya umekuwa ukiahirishwa mara kwa mara.
Suala hili limesababisha vurugu na maandamano ya raia wa DRC ambao hata hivyo inaelezwa kuwa wamekuwa wakipigwa na askari polisi jamabo ambalo kwenye taarifa ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa December 31, 2017 imelaani vikali vitendo hivyo.
Wiki iliyopita Kanisa katoliki nchini DRC waliandamana kushinikiza kuachia madaraka kwa rais huyo katika mji wa Kinshasa.
Katika maandamano hayo jijini Kinshasa watu watano waliuawa na polisi siku hiyo kwenye maandamano hayo.