Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Irene Uwoya amesema kuwa hawezi kuusahau mwaka 2017 kwani amekumbana na vitu vingi maishani mwake kuliko mwaka wowote.

Uwoya amesema kuwa mwaka uliopita ni moja ya mwaka ambao ameweza kupitia mambo mengi ambayo hatoyasahau kuliko mwaka mwingine wowote.

Irene amesema hayo na kuthibitisha kuwa 2017 ni moja ya miaka yake ambayo mambo mengi yametokea na yamemfanya aweke historia.

Muigizaji huyo amesema kuwa kuna mwaka ambao mambo mengi yanaweza kukutokea na yapo yatakayokuwa mazuri sana au mabaya sana , lakini kwa upande wake mwaka 2017 ulikuwa n mwaka wa maumivu kutokana na kuumizwa na badhi ya matukio ikiwemo lile la kumpoteza aliyekuwa mume wake wa ndoa Hamad Ndikumana Kataut.

Mwaka uliopita irene alikuwa ni moja ya wasanii wa kike walisema sana katika mitandao ya kijamii kutokana na atukio mengi yalikuwa yakimtokea, ambapo alimpoteza mume wake na kifo hicho bado kilisemekana kuwa kimesababishwa na yeye mwenyewe kutokana na kuolewa na mwanaume mwingine bila kupeana talaka na  mumewe huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *