Askari Polisi aliyempiga risasi mpenzi wake, Zakayo Dotto Kileka amejisalimisha katika kituo cha Polisi Mkonai Njombe.

Mdogo wa marehemu ambaye alikua akiishi nae ameeleza kuwa Zakayo alimfumania dada yake Neema akiwa amelala na mwanaume mwingine na ugomvi mkubwa ulitokea baada ya kuona kazidiwa, Zakayo aliamua kutumia silaha.

Hata hivyo katika harakati za kumsaka mtuhumiwa huyo, Pc Zakayo amejisalimisha kituo cha polisi Makambako asubuhi leo majira ya saa moja na nusu.

Alionekana katika vazi lake la uniform likiwa limelowa damu, lakini pia koromeo lake lameonekana kama mtu alietaka kujizuru.

Neema alikua akifanya kazi JWTZ Camp ya Makambako na Zakayo akiwa ni  Polisi Makambako katika ofisi za banki ya NMB.

Mwili wa marehemu Neema umehifadhiwa katika hospitali teule ya Ilembula baada ya kufanyiwa Pm katika hospitali ya mji Makambako. Neema ataagwa leo tayari kwa kuurejesha mwili makwao kwa maziko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *