Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji amewataka vijana kuacha kulalamika ifikapo mwaka 2018 ili kufikia malengo yao.
Dewji amewasihi Watanzania kama wanaona hawapendezwi na kitu fulani njia nzuri ni kukibadili kitu hicho na kuacha kulalamika kwani hakutaweza kubadili jambo lolote lile.
Kupitia mtandao wake ameandika “Kama hupendi kitu fulani, (jaribu) kibadilishe! Unataka kupunguza uzito? Badilisha milo yako, fanya mazoezi. Unataka kukutana na watu wapya? Toka nje, tembea na jichanganye na watu wengine! Kumbuka kulalamika hakubadilishi jambo usilolipenda!”.
Mapema mwaka huu mfanyabishara huyo kijana aliibuka mshindi wa tuzo ya mtu aliyefanya vizuri katika Uongozi kwa Mwaka 2016 inayotolewa na Jarida la African Leadership.
Dewji alitunukiwa rasmi tuzo hiyo katika sherehe itakayofanyika Februari 24, mwaka huu katika Hoteli ya Southern Sun mjini Pretoria nchini Afrika Kusini.