Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Baraka The Prince amefunguka na kusema kuwa atatoa kiasi cha milioni tatu kwa atakayemgundua mtu anayemfanyia hujuma kwenye mtandao wake wa ‘Youtube’.
Baraka amesema kuwa amechoshwa na mtu huyo kwani amekuwa akiamfanyia hujuma katika mtandao wake wa ‘Youtube’ kila akiweka video zake mpya.
Baraka awali alikuwa akilalamika akionyesha kuwa mtu ambaye anamfanyia hujuma hizi anamtambua kuwa ni moja kati ya viongozi wake ambao walikuwa wakimsimamia katika kazi zake za muziki.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kuwa “Kwanza nishukuru sana mashabiki zangu mnaojitahidi kunipigania na kupoteza muda wenu kwa ajili ya kazi lakini kuna mtu mmoja tu ambae aliumbwa kurudisha nyuma hatua za watu. Kila siku ‘viwes’ wanazidi kupungua sasa basi natangaza kumpa zawadi ya Tsh Milioni 3 kwa yeyote atakayetuthibitishia na kutuletea uyu mtu”.
Pia ameendelea kuandika “Maana huku ni kudharau kazi yangu na kudharau muda wa mashabiki zangu, Radio na Tv na vyombo vyote vya habari ambavyo vimenipigania takribani miaka 5 sasa nikiwa katika tasnia ya bongo fleva”.