Kocha wa Manchester United Jose Mourinho analenga kumsajili kiungo wa kati wa Argentina Paulo Dybala, 24, katika dau la £60m kutoka Juventus.
Wakati huohuo manchester United imeimarisha dau lake kwa kiungo wa kati Marouane Fellaini, ili kumzuia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 ambaye I yake inakamilika mwishoni mwa msimu huu.
United pia imeanza mazungumzo na mshambuliaji wa Bordeaux ,20, Malcom, huku mkufunzi Jose Mourinho akiajindaa ku;ipa dau la £33m.
Arsenal wameambia kwamba ni lazima walipe dau la £40m kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani Julian Draxler, 24, kutoka Paris St-Germain.
Image caption Arsenal wameambia kwamba ni lazima walipe dau la £40m kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani Julian Draxler, 24, kutoka Paris St-Germain.
The Gunners wako katika ushindani mkali na Liverpool wa kutaka kumsajili mshambuliaji wa PSV Eindhoven Hirving Lozano mwenye umri wa miaka 22, ambaye ana thamani ya £42m
Hatahivyo usajili wa mchezaji huyo wa hadi £35m utaifanya Arsenal kumuuza mshambuliaji wake Alexis Sanchez, 29, mnamo mwezi Januari.
Kocha Antonio Conte ameitaka usimamizi wa Chelsea kuwasajili wachezaji watatu wapya mnamo mwezi Januari.
Kocha mpya wa West Ham David Moyes ana hamu ya kumsajili Steven Nzonzi iwapo Sevilla itaamua kumuuza mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29 mwaka ujao.
Celtic Imekana madai kwamba imekubali ombi la £18m kumuuza mshambuliaji Moussa Dembele, 21, kutoka.
Mkufunzi Roy Hodgson anahofia kwamba Crystal Palace italazimika kumuuza Wilfried Zaha mwezi ujao huku Manchester City, Chelsea na Tottenham zote zikimtaka winga huyo ,25.
Uingereza inatarajiwa kucheza mechi ya kujiandaa katika uwanja wa Leeds huku meneja Gareth Southgate akataka kuungwa mkono kabla ya michunao ya kombe la dunia ya 2018 nchini Urusi.
Mkufunzi wa Everton Sam Allardyce amefichua kwamba aliisaidia kuimarisha motisha ya mabeki Michael Keane na Ashley Williams kupitia usaidizi wa mchezo wa runinga wa The Cube.