Mwanasheria mkuu wa chama upinzani Chadema, Tundu Lissu, ameweza kusimama kwa mara ya kwanza baada ya kushambuliwa.

Tundu Lissu amekuwa akipokea matibabu Nairobi tangu alipopigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma mwezi Septemba.

Katika picha iliowekwa katika ukurasa wa Facebook wa CHADEMA, mbunge huyo anaonekena akisimama akisaidiwa na wahudumu wawili wa hospitali.

Ujumbe ulioambatana na picha ukisema “Wiki iliyopita niliwataarifu kwamba madaktari wangu wamesema ‘nitasimama, nitatembea na nitarudi Tanzania.

Leo Boxing Day nimeweza kusimama kwa mguu mmoja kwa msaada wa ‘Mababa Cheza’ wangu. Hatua inayofuata ni magongo kesho na nitawajulisheni hatua nyingine katika matibabu yangu.

.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *